Thursday, July 16, 2015

Nyumba ya Chriss Brown yavamiwa

Nyumba ya Chris Brown Marekani imevamiwa na kupekuliwa na watu watatu waliofunika nyuso zao ambao walimfungia shangazi wake ndani ya chumba chake
kwa maelezo ya maafisa wa polisi.

Chriss Brown hakuwepo nyumbani kwake wakati wa wizi huo ambao ulifanyika alfajiri siku ya jumatano.
Maafisa wanasema kuwa washukiwa ambao walikuwa na bunduki waliondoka katika jumba hilo la Tarzana na fedha za kiasi kisichojulikana pamoja na vitu kadhaa vya binafsi.

Brown hajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.
Kulingana na ripoti kutoka Marekani Brown alikuwa Hollywood Nite Club wakati ishu hyo inatokea.

Hii ni mara ya pili ya nyumba ya Chriss Brown kuvamiwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.
Mwezi Mei, aliwasili nyumbani na kumpata mwanamke mmoja aliyedaiwa kuvunja na kuingia kupika vyakula kadhaa na kuandika ukutani kwamba anampenda msanii huyo

0 Comments:

Post a Comment