Hotuba ya Kambi ya upinzani kuhusu bajeti ya ofisi ya Waziri
Mkuu, haitasomwa bungeni baada ya kambi hiyo kuchelewa kuiwasilisha.
Hayo
yameelezwa leo, Aprili 4 na Naibu Spika Dk Tulia Ackson dakika chache
kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kusoma bajeti yake.
“Kwa
maelekezo yaliyotolewa na Spika Ndugai, kwa kambi ya upinzani ni kuwa
upinzani wanatakiwa kuwasilisha hotuba yao siku moja kabla ya bajeti
kusomwa bungeni ili kuondokana na matatizo ya kuchelewa kuzipata hotuba
hizo,” amesema Dk Ackson
Waziri Majaliwa leo anawasilisha bungeni
mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na
matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge, kwa mwaka
wa fedha 2018/2019 mjini Dodoma.
Wednesday, April 4, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment