WINGA
wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva leo amefunga mabao mawili timu
yake, Difaa Hassan El Jadida ikilazimisha sare ya 3-3 ugenini katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco dhidi ya wenyeji, Olympique de Khouribga
Uwanja wa Phosphate mjini Khouribga.
Matokeo
hayo yanaiongezea pointi moja Jadida na kushuka kwa nafasi moja hadi ya
nne kwenye Ligi ya Morocco yenye timu 16, ikifikisha pointi zake 38
baada ya kucheza mechi 25.
Msuva
amefunga mabao yake dakika za 65 na dakika ya pili ya muda wa nyongeza
baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, hilo likiwa bao lililoinusuru
Jadidi kupoteza mechi leo na kuibuka shujaa wa timu yake, wakati bao
lingine la timu hiyo limefungwa na Tarik Astati dakika ya 33.
Mabao ya Khouribga yamefungwa na Zouhair El Moutaraji mawili dakika za nne na 38 na Adam Nafati dakika ya 55.
Kikosi
cha Difaa Hassan El-Jadida kilikuwa; Aziz El Qinani, Fabrice Ngah,
Youssef Aguerdoum, Tarik Astati, Mohamed Hamami, Bakary N'diaye,
Marouane Hadhoudi, Bilal El Magri, Saimon Msuva, Ayoub Nanah na Mario
Mandrault Bernard.
0 Comments:
Post a Comment