Wateja wa mafuta wakisubiri foleni ya mafuta Mkoani Njombe, Nishati Hiyo Imekuwa kitendendawili kwa siku za hivi karibuni.
Sunday, October 28, 2012
Saturday, October 13, 2012
MRADI WA KILIMO WAZINDULIWA WILAYANI WANGING'OMBE
Mradi wa mwelekeo wa maendeleo ya kilimo katika shirika la
maendeleo ya kilimo mkoa wa Njombe la NADO
unaoitwa NADO IN FOCUS leo umezinduliwa rasmi Wilayani Wanging'ombe.
Akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Njombe
Afisa Biashara wa mkoa wa Njombe bwana George Lupembe amepongeza jitihada kubwa
zinazofanywa na shirika la NADO Katika kuwakomboa wakulima kwa kujiinusuru na
kipato kupitia kilimo ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza Sera ya KILIMO
KWANZA hapa Nchini.
Bwana Lupembe amesema kuwa pamoja na kuzindua mradi huo
ulioambatana na uzinduzi wa vyombo vya usafiri kwa maafisa kilimo lakini
serikali haina budi kuendeleza ushirikiano na shirika hilo ili kupunguza ukali
wa maisha kwa wakulima mkoani Njombe
Friday, October 12, 2012
WAFANYABIASHARA WALAZIMIKA KUAHIRISHA KIKAO NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA
Baadhi ya Wafanyabiashara Mjini Njombe Wakiwa Nje ya Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Wafanyabiashara Mijini Njombe Wamelazimika Kuahirisha Kikao Kilichopangwa Kufanyika Saa 3 Asubuhi Hii Leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwa. Valency Kabelege Baada ya Mwenyekiti Huyo Kutoa Taarifa ya Kuwa na Dharura Ndani ya Muda wa Kikao Hicho.
Kikao Kilichopangwa Kufanyika Saa 3 Asubuhi Hii Leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwa. Valency Kabelege Baada ya Mwenyekiti Huyo Kutoa Taarifa ya Kuwa na Dharura Ndani ya Muda wa Kikao Hicho.
Akitoa Taarifa Hiyo Kwa Njia ya Simu, Bwa. Kabelege Alisema Kuwa Yupo Kwenye Kikao Lakini Muda Mfupi Baadae Alitoa Taarifa Tofauti Kupita Kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuwa Mtoto Wake ni Mgonjwa Hivyo Hatoweza Kuhudhuria.
Kikao Hicho Kimeahirishwa Mpaka Tarehe 16 Mwezi Huu Saa 3 Asubuhi Kikao Ambacho Kitawahusisha Wawakilishi wa Wafanyabiashara Hao Wakiongozwa na Mwenyekiti Patrick Msigwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwa. Kabelege.
Siku ya Jumanne ya Tarehe 09 Mwezi Huu Wafanyabiashara Hao Walifanya Kikao na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Wakiwasilisha Madai Yao Kwa Serikali Kwa Kushindwa Kulipwa Madai Yao Kwa Wakati.
Katika Kikao Hicho Kilichopita Bwana Mwanzinga Alikiri Kuwepo Kwa Tatizo Hilo na Kuahidi Kulitolea Ufafanuzi Siku Ya Tarehe 13 Jumamosi Mwezi Huu Saa 6 Mchana Katika Ukumbi wa PASTO Mjini Njombe.

Thursday, October 11, 2012
HALI YA UPATIKANAJI WA MAFUTA YAREJEA KAWAIDA MJINI NJOMBE
Hali ya Upatikanaji wa Mafuta Katika Mji wa Njombe Imerejea Katika Hali ya Kawaida Baada ya Siku Kadhaa Zilizopita Kutopatikana kwa Nishati Hiyo Muhimu Hasa Mafuta Aina ya Dizeli.
Akiongea na Mwandishi wa Blog Hii, Meneja wa Kituo cha Kuuza Mafuta cha Ndime, Clement Mwauling'ombe Mtewele amesema kuwa Mafuta aina ya Dizeli yameanza Kupatikana Tangu Jana na kiasi cha mafuta kilichopo kwa sasa kinaridhisha
kutegemeana na mahitaji ya wateja wake.
Pia Bwana Mtewele Hakusita Kuimwagia Sifa
Uplands Radio Kwa Kutoa Matangazo Na Vipindi
Vizuri Vya Kuburudisha na Kuelimisha Umma
Kwa upande wake Msemaji wa Kituo cha Gapco, Bi Joyce Fute Amesema mafuta Yanapatikana kwa Wingi Kituoni Hapo Tangu Jana. Pia Bi Fute Amewaondoa Hofu Watumiaji Wa Nishati Hiyo Kwa Kuwa Wana Hifadhi ya Kutosha kwa Sasa. Pamoja na Kuwa Vituo Vingi Kuonekana
Kupatikana
Mafuta Hivi Sasa Lakini Baadhi ya Vituo Vimeonekana Kufungwa
Muda Wote Kama Vile
Oilcom na Wahudumu Wake Kutopatikana
Tuesday, October 2, 2012
Wanafunzi 25 wauawa na Boko Haram
2 Oktoba, 2012 -

Abubakar Shekahu kiongozi wa kundi la Boko Haram
Zaidi ya wanafunzi 25 wameuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Mubi, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Polisi wamefahamisha kuwa shambulizi hilo limetokea katika mabweni yao mbali kidogo na chuo cha ufundi anuwai cha Mubi.Mhadhiri mmoja amefahamisha kuwa wanafunzi 40 wameuawa lakini bado taarifa hizo hazijathibitishwa.
Mauaji haya yanakuja siku chache baada ya operesheni kali kufanywa dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram mjini humo.
Aidha mhadhiri ambaye hakutaka kutajwa, aliambia kwamba wanafunzi waliamrishwa kupanga foleni na kusema majina yao mmoja baada ya mwingine kabla ya kuuawa.
Haijulikani kwa nini baadhi waliuawa na wengine kuachwa, baadhi ya wale waliouawa ni waisilamu.
"kila mtu anaogopa na wamejifungia vyumbani," alisema mhadhiri huyo.
Aliongeza kuwa wanafunzi sasa wameanza kuuhama mji huo. Inasemekana wameweka majani ya rangi ya kijani kibichi kwenye magari yao kama ishara kuwa hawaungi mkono upande wowote.
Wapiganaji wa Boko Haram wanaopigana wakitaka sheria za kiisilamu kutumika, wamewaua zaidi ya watu 1,000 Kaskazini mwa Nigeria.
Subscribe to:
Comments (Atom)