Mradi wa mwelekeo wa maendeleo ya kilimo katika shirika la
maendeleo ya kilimo mkoa wa Njombe la NADO
unaoitwa NADO IN FOCUS leo umezinduliwa rasmi Wilayani Wanging'ombe.
Akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Njombe
Afisa Biashara wa mkoa wa Njombe bwana George Lupembe amepongeza jitihada kubwa
zinazofanywa na shirika la NADO Katika kuwakomboa wakulima kwa kujiinusuru na
kipato kupitia kilimo ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza Sera ya KILIMO
KWANZA hapa Nchini.
Bwana Lupembe amesema kuwa pamoja na kuzindua mradi huo
ulioambatana na uzinduzi wa vyombo vya usafiri kwa maafisa kilimo lakini
serikali haina budi kuendeleza ushirikiano na shirika hilo ili kupunguza ukali
wa maisha kwa wakulima mkoani Njombe
.
.
Afisa huyo wa biashara katika mkoa wa Njombe aliyemwakilisha
mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi amewataka wakulima katika
shirika la NADO kumuunga mkono mkulima ambaye ni mzalishaji na msambazaji wa
mbegu za mazao katika wilaya ya Wanging'ombe
bwana Njogela mkulima wa kijiji cha Chalowe kwa kuzinunua ili kuendana na kasi
ya kilimo katika Halmashauri zote za mkoa wa Njombe.
Akitoa taarifa ya shirika hilo la NADO pamoja na mradi huo Mkurugenzi wa
shirika hilo bwana John Wihallah amesema kuwa Shirika hilo ni matokeo ya
mwendelezo wa umoja wa vikundi vya maendeleo katika vijiji vya
Sakalenga,Palangawanu,Chalowe na Itulahumbavilivyoanza kufanya shughuli za maendeleo ya jamii na MS Tanzania mwaka 1996
kwa ubia.
Wihallaha amesema mradi huo uliozinduliwa rasmi leo
umefadhiliwa na shirika la maendeleo ya kilimo la Denmark na Asia utakao kuwa
na kipindi cha miaka mitatu wenye gharama zisizo pungua shilingi bilioni tatu kwa ajili ya mafunzo ya
mazao ya mazao ya Alizeti,Maharage,Mahindi,Kabeji,Nyanya na viazi mviringo
ukiwa na lengo la kuwafikia wakulima 9000 katika vijiji 200 ifikapo 2015.
Mradi huo umeambatana na uanzishwaji SACCOS,Darasa la
kompyuta,utengenezaji wa Batiki na sabuni,usindikaji wa matunda,Mbogamboga na
vyombo vya usafiri kama pikipiki zenye gharama ya shilingi milioni 35 pamoja na
usajili kuwa za NADO likiwemo gari la mradi na vitendea kazi vya ofisi na
mawasiliano.
0 Comments:
Post a Comment