Hali ya Upatikanaji wa Mafuta Katika Mji wa Njombe Imerejea Katika Hali ya Kawaida Baada ya Siku Kadhaa Zilizopita Kutopatikana kwa Nishati Hiyo Muhimu Hasa Mafuta Aina ya Dizeli.
Akiongea na Mwandishi wa Blog Hii, Meneja wa Kituo cha Kuuza Mafuta cha Ndime, Clement Mwauling'ombe Mtewele amesema kuwa Mafuta aina ya Dizeli yameanza Kupatikana Tangu Jana na kiasi cha mafuta kilichopo kwa sasa kinaridhisha
kutegemeana na mahitaji ya wateja wake.
Pia Bwana Mtewele Hakusita Kuimwagia Sifa
Uplands Radio Kwa Kutoa Matangazo Na Vipindi
Vizuri Vya Kuburudisha na Kuelimisha Umma
Kwa upande wake Msemaji wa Kituo cha Gapco, Bi Joyce Fute Amesema mafuta Yanapatikana kwa Wingi Kituoni Hapo Tangu Jana. Pia Bi Fute Amewaondoa Hofu Watumiaji Wa Nishati Hiyo Kwa Kuwa Wana Hifadhi ya Kutosha kwa Sasa. Pamoja na Kuwa Vituo Vingi Kuonekana
Kupatikana
Mafuta Hivi Sasa Lakini Baadhi ya Vituo Vimeonekana Kufungwa
Muda Wote Kama Vile
Oilcom na Wahudumu Wake Kutopatikana
0 Comments:
Post a Comment