Baadhi ya Wafanyabiashara Mjini Njombe Wakiwa Nje ya Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Wafanyabiashara Mijini Njombe Wamelazimika Kuahirisha Kikao Kilichopangwa Kufanyika Saa 3 Asubuhi Hii Leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwa. Valency Kabelege Baada ya Mwenyekiti Huyo Kutoa Taarifa ya Kuwa na Dharura Ndani ya Muda wa Kikao Hicho.
Kikao Kilichopangwa Kufanyika Saa 3 Asubuhi Hii Leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwa. Valency Kabelege Baada ya Mwenyekiti Huyo Kutoa Taarifa ya Kuwa na Dharura Ndani ya Muda wa Kikao Hicho.
Akitoa Taarifa Hiyo Kwa Njia ya Simu, Bwa. Kabelege Alisema Kuwa Yupo Kwenye Kikao Lakini Muda Mfupi Baadae Alitoa Taarifa Tofauti Kupita Kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuwa Mtoto Wake ni Mgonjwa Hivyo Hatoweza Kuhudhuria.
Kikao Hicho Kimeahirishwa Mpaka Tarehe 16 Mwezi Huu Saa 3 Asubuhi Kikao Ambacho Kitawahusisha Wawakilishi wa Wafanyabiashara Hao Wakiongozwa na Mwenyekiti Patrick Msigwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwa. Kabelege.
Siku ya Jumanne ya Tarehe 09 Mwezi Huu Wafanyabiashara Hao Walifanya Kikao na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Wakiwasilisha Madai Yao Kwa Serikali Kwa Kushindwa Kulipwa Madai Yao Kwa Wakati.
Katika Kikao Hicho Kilichopita Bwana Mwanzinga Alikiri Kuwepo Kwa Tatizo Hilo na Kuahidi Kulitolea Ufafanuzi Siku Ya Tarehe 13 Jumamosi Mwezi Huu Saa 6 Mchana Katika Ukumbi wa PASTO Mjini Njombe.
Friday, October 12, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment