Saturday, February 11, 2017

'Acheni WIVU fungueni AKILI' Kauli Ya Professor Jay kwa WanaHipHop

Post ya Prof Jay baada ya kuona post ya Nash Mc

Juzi tu dogo Nash Mcee aliuliza hivi SINGELI imeshakwenda international? Nilitegemea angeuliza kwa nini HIPHOP Ya Bongo haivuki Boarder? Mkafurahia KISHABIKI bila kujiuliza HIPHOP ndio imezaa karibu aina zote za muziki wa kizazi kipya lakin mbona wasanii wake hawafiki mbali? Matokeo yake baadhi ya wasanii wanaojiita wa HIPHOP na mashabiki wao wanaichukia aina nyingine ya muziki kwa mafanikio wanayopata wenzao. Badala ya kujiuliza tumekosea wapi sasa tunakuwa na WIVU wa kijinga na kuchukia mafanikio ya wengine waliopambana kufika hapo walipo sasa. Kupinga MTU aliyefanikiwa hakukupi uhalali wa wewe kufanikiwa, Tuna nafasi ya kujirekebisha na kupeleka HIPHOP Yetu mbali ila sio kwa WIVU.
MAPINDUZI yaliyofanywa na Kwanza unit, Saleh Jabri, Hbc, Sugu, Hashim, Majani, GWM, Solo, Afande, Jmo nk yalifanikiwa kwa UPENDO sio CHUKI. Hata wanaojitahidi kupeperusha bendera ya HipHop kama@TheRealFidQ @JohMakinitz watu wanawakatisha tamaa, I RESPECT YOUR HUSTLE my young brothers. Matokeo yake hao wanaopinga wenzao wanaoonyesha JUHUDI, wanaishia kuimbia washkaji zao kwenye vibanda vya kahawa, U NEED TO GROW Up.
Kizazi hiki cha HIPHOP Kimekuwa kama Ukoo wa KAMBALE Baba, Mama na watoto wote wana NDEVU, Kila MTU akiambiwa mkali anajiona kweli KAMALIZA. Hii Heshima mliyoikuta kwenye HIPHOP tuliitafuta kwa Jasho na Damu kisha mnaichukulia poa tu, Badala ya kwenda mbele mnarudi nyuma kwa kasi. Wakati ule TANZANIA tulikuwa wa pili Africa tukishindana na SENEGAL ya kina DIDIER AWADI ila sasa hata Sudan wanatukimbiza, HAMJIULIZI tu?
Tumebaki kujazana ujinga kwenye vijiwe vyetu na kujifanya REAL HIPHOP wkt hakuna chochote mnachokifanyia HIPHOP, Acheni WIVU fungueni AKILI.

0 Comments:

Post a Comment