Tuesday, April 18, 2017

Baba mzazi wa Belle 9 afariki kwa ajali

Baba mzazi wa Belle 9 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, baada ya kupata ajali ya kugongwa na pikipiki mkoani Morogoro.


Mzee Damian alivunjika mguu katika ajali hiyo na kupata majeraha mengine mabaya yaliyopelekea kifochake.

Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo kasi wa pikipiki, majeruhi alikimbizwa hospitali na kuwekwa katika wodi ya wagonjwa mahututi lakini alikosa dawa kwa wakati kitu ambacho kilishindwa kuokoa uhai wake. Jahz Zamba ambaye ni meneja wa Belle 9 amethibitisha na kusema kaka yake Belle anayeishi Morogoro aliingia mtaani kuzisaka na aliporudi mida ya saa sita usiku alikuta Mzee ameshafariki.
Dereva wa pikipiki hiyo naye amejeruhiwa vibaya.

The Sametype inatoa pole kwa familia ya Mzee Damiani. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amina 

0 Comments:

Post a Comment