Tuesday, April 18, 2017

Zadane asisitiza kulinda ushindi dhidi ya Bayern





Kocha wa Real Madrid amewasisitiza wachezaji wake kuwa bado wanahitaji kuwa bora ili kulinda ushindi walioupata kutoka kwa Bayarn wiki iliyopita.


Real Madrid inawakaribisha Bayern Munchen katika mechi yamarudiano ya ligi ya mabingwa hatua ya robo fainali itakayopigwa saa 3:45 usiku kwa saa za afrika mashariki.

Bayern inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza nyumbani kwa 2-1 huku Arturo Vidal akiifungia Bayern goli la pekee na kukosa penati. Katika mechi hiyo pia mshambuliaji wa Real Madrid aliweka rekodi ya kupachika mabao 100 katika ligi hiyo baada ya kufunga magoli mawili yaliyowapa ushindi wa ugenini Madrid.

Mechi nyingine inayopigwa leo ni kati ya Leicester wanaowakarisha Atletico ya Hispania. Leicester ililala kwa bao moja dhidi Atlletico katika mechi iliyopita.

0 Comments:

Post a Comment