Leo
July 26, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kusikiliza
maombi ya dhamana yaliyotolewa na Mfanyabiashara
maarufu Tanzania Yusuf Manji,
August 4, 2017.
Jaji
Isaya Arufani amesema hayo baada ya Mawakili wa Serikali Paul Kadushi na Simon
Wankyo kuyapokea maombi hayo na kusema wana nia ya kuyapinga huku Jaji akisema
anakubaliana na hoja zao na August 4, 2017 maombi hayo ya dhamana yataanza
kusikilizwa.
Katika
maombi hayo Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana
iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya
akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
0 Comments:
Post a Comment