Mahakama moja nchini
Korea Kusini imemhukumu kifungo cha miaka
mitano jela Mkurugenzi Mkuu na mrithi wa
Samsung, Lee Jae-yong baada ya kutiwa hatiani kwa
rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.
Lee alishtakiwa kwa tuhuma za rushwa akidaiwa
kutoa msaada wenye thamani ya Dola 36 milioni za
Marekani kwa taasisi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa na Choi Soon-sil ambaye ni rafiki wa Rais wa
zamani wa Korea Kusini, Park Geun-hye kwa malengo ya kujipatia faida kisiasa.
Kutokana na tuhuma hizo za rushwa, Lee alikamatwa na kuwekwa kizuizini tangu Februari. Kashfa
hiyo ilisababisha maandamano ya wananchi kumpinga Rais Park aliyeondolewa madarakani.
Mwanasheria wa Lee, Song Wu-cheol amesema kuwa wanatarajia kukata rufaa kupinga hukumu hiyo
wakiamini mahakama inaweza kuitengua.
Friday, August 25, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment