Serikali imesema ipo tayari kugharamia gahrama za matibabu ya Mbunge wa
Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu katika hospitali yoyote duniani, iwapo
familia itaomba jambo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , na kusema kwamba kama familia
itahitaji na ripoti ya madaktari ikionyesha kuna ulazima, serikali itasimamia
suala hilo.
Hivi karibuni kumekuwa kukiendeshwa kampeni ya kuchangia matibabu ya Tundu
Lissu baada ya gharama zake za matibabu kuwa kubwa huku watu wakiitupia lawama
serikali.
Thursday, September 21, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment