Msigwa
ameachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao ni Alex Kimbe
pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa Leonce Marto , saa nne usiku
Msigwa alishushwa jukwaani jana jioni na
jeshi la polisi akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya
Mlandege Manispaa ya Iringa ambapo alikamatwa kwa kutuhumiwa kufanya
uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .
Inadaiwa kuwa Mchungaji Msigwa alikuwa na kibali cha siku tatu cha kufanya mikutano katika jimbo lake na mkutano wa jana ulikuwa wa kwanza.
Marto amesema mikutano yake imefungiwa
na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine mpaka hapo OCD
atakapoamua au vinginevyo.
Leo mbunge Peter Msigwa anatakiwa
kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari
imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa Mahakamani .
Imebainishwa kwamba mbunge huyo
atazungumza na vyombo vya habari leo mchana kuweka wazi madhila
yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.
0 Comments:
Post a Comment