Sunday, September 16, 2012

                                   Pipi sasa ni mama 

Pipi baada ya kujifungua
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Pipi ambaye alifanya vizuri katika wimbo wa "Njia Panda" alioshirikiana na Barnaba amebahatika kuitwa Mama baada ya kujifunga mtoto wa kiume aliyempa jina Kingston siku ya tarehe 14 septemba mwaka huu.


    Baada ya kujifungua Pipi alimshukur Mungu kwa kutimiza lake la kuzaa kwa uchungu, lakini pia hakusita kumshukuru mama yake


     Tunakutakia malezi mema na yenye maadili kwa mtoto wako Kingston kwani MKONO ULEAO MWANA NDIO UJENGAO TAIFA.

0 Comments:

Post a Comment