Tuesday, September 11, 2012

TEC wachangia maoni kuelekea siku ya maadhimisho Tabaka Anga Hewa

           Wanafunzi wa chuo cha Tanzania e College jana walifanya intavyuu kuchangia maoni yao kuhusiana na mkutano wa 14 wa kimataifa wa Tabaka Anga Hewa unaoendelea Arusha. Tanzania imepata heshima ya kuandaa mkutano ikiwa ni sehemu ya kujadili matatizo na madhara yatokanayo na uharibifu wa anga hewa.
            Katika intavyuu hiyo iliyofanya na mwandishi wa habari wa TBC TAIFA, Musa Twangilo, wanafunzi hao walieleza sababu zinazopelekea kuharibu tabaka la Anga Hewa ambapo kunachangia madhara makubwa kwa viumbe hai hapa duniani.
             Wanafunzi hao walizitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na ongezeko la viwanda vinavyozalisha moshi wenye kemikali zinazopelekea mvua za asidi (Acidic Rains) na ukataji wa miti hovyo. Pia wataja madhara yake kuwa ni kuongezeka kwa joto, mabadiliko ya majira ya mvua na ukame. Walioingeza madhara mengine kuwa ni magonjwa yatokanayo ongezeko la joto, kupotea kwa baadhi ya viumbe hai na mvua zisizo tarajiwa.
             Siku ya Tabaka Anga Hewa huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 mwezi Septemba duniani kote kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira ili kutunza tabaka anga hewa. 

0 Comments:

Post a Comment