Friday, November 30, 2012

SERIKALI YATAKIWA KUONGEZA BAJETI YA MAHAKAMA

 Serikali Imetakiwa  Kuongeza  Bajeti Katika Idara ya Mahakama  Hapa Nchini Ili Kuepuka  Vitendo Vya Rushwa Kwa  Wananchi  Waendeshaji  Mahakama.

Akizungunza na Kituo  Hiki Mwanasheria John Owegi  Ambaye ni Wakili wa Kujitegemea Mkoani Njombe Anesema Ufinyu Wa Bajeti  Katika Mahakama Unapelekea Kuwepo Kwa Mianya ya Rushwa na Kukosesha Haki Kwa  Mtuhumiwa Hali Inayo Pelekea Kupindishwa Kwa Sheria Miongoni Mwa Jamii.

Bwana Owegi Amesema Kuwa Hali Hiyo Inapelekea Kuvunjika Kwa Amani Hapa Nchini  Kutokana na Baadhi ya  Mahakama  Kutotenda Haki Katika Maamuzi ya Kazi na Hivyo Kuleta  Mpasuko  wa Kisheria Kwa Wananchi.

Aidha Amewataka Wananchi Kuwatumia  Mawakili Wa Kujitegemea Katika  Kazi Zao Kutokana  na Mahakama  Kushindwa  Kutenda Haki  Katika Maamuzi  Hali Inayopelekea Kuhukumiwa Kwa Mtu Ambaye  Wakati Mwingine Hana Hatia.

Akijibu Swali Lililouliza Juu ya  Utaratibu Wa  Kutumia Wakilia wa Kujitegemea  Wakili Owegi Amewataka Wananchi Kuondoa  Hofu Juu ya Huduma Zao Kwani Wakati Mwingine Wao Hutoa Huduna ya Kisheria Bure  Kulingana  na Ukubwa wa Kasi  na Kwamba Wao Wapo Kwaajili ya Jamii Hivyo Kinachopelekea  Kumchaji mteja ni  kutokana na wao kulipia leseni.

SERIKALI INATARAJIA KUZINDUA CHANJO MPYA MBILI ZA WATOTO WACHANGA

Serikali inatarajia kuzindua chanjo mpya mbili za watoto wachanga ikiwemo chanjo ya kuzuia kuharisha na chanjo ya kichomi NIMONIA ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayeitwa STREPTOCOCCUS PNEUMONIAE Ulioonekana kuwakumba watoto wadogo.

Akifungua kikao cha semina ya afya ya Mkoa wa Njombe iliyolenga kutoa elimu juu ya chanjo hizo mkuu wa mkoa
 wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi amewataka wazazi kumpeleka mtoto kupata chanjo hizo kabla ya siku saba baada ya kuzaliwa kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kwa mtoto kutokana na kukosa chanjo hizo.

Captain Msangi ameeleza kuwa wataalamu wa afya hawana budi kutoa elimu ya kiwango cha juu kwa wauuguzi watakao husika na zoezi hilo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwani chanjo hususani za sindano zinahitaji umakini mkubwa wakati wa kumchoma mtoto.


Akitoa elimu hiyo kwa  wadau mbalimbali wa afya katika ngazi ya mkoa wa Njombe Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Thomas Lujuo amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Ugonjwa wa Kuhara Umekuwa Ukishika Nafasi ya Pili Kati ya Magonjwa Yanayoongoza Kwa Kusababisha Vifo Vya Watoto Kwa Asilimia 17 Huku Ugonjwa wa Nimonia Ukisababisha Vifo Kwa Asilimia 14 Ulimwenguni Kote.

Dokta Lujuo ameeleza baadhi ya dalili za ugonjwa wa NIMONIA Kuwa ni pamoja na mtoto kupumua kwa shida,kukohoa,homa na kushindwa kula au kunyonya.

Aidha Dokta huyo amesema NIMONIA husababisha vifo zaidi ya milioni 1.4 duniani kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano huku kwa nchi za afrika,NIMONIA huchangia asilimia 18% ya watoto waliochini ya umri wa miaka  mitano.

Amesema Kuwa Chanjo Hiyo Ni Kampeni ya Kitaifa Inayotokana na Tafiti za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Kuonesha kuwa Watoto wengi wanapata Magonjwa ya Kuhara Na Nimonia .



Thursday, November 29, 2012

Wednesday, November 28, 2012

WAFANYABIASHARA WALALAMIKIA KODI YA MISITU

Msako wa kodi zitokanazo na misitu uliofanyika kuanzia novemba 26 mwaka huu mjini Njombe umepelekea malalamiko makubwa kwa wafanyabiashara kuilalamikia serikali kwa kuendesha zoezi hilo kwa kutumia nguvu.

 Hali hiyo imepelekea wafanyabiashara wa bidhaa zitokanazo na misitu ya maliasili kuingiwa na hofu kubwa kutokana na msako huo uliofanyika kwa kutumia jeshi la polisi ambao wamekuwa wakitumia silaha za moto huku wakisema zoezi hilo limefanika ghafla bila mawasiliano.

 Wakizungumza kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Turbo baina ya Wafanyabiashara hao na maliasili wamesema kuwa hatua ya kuwakamata kulipia kodi bila kuangalia uwezo wa biashara ni kuwanyanyasa na kuwanyima haki za kufahamu sheria ya tozo la kodi hizo.

Wamesema kuwa kitendo cha Halmashauri ya mji wa NJOMBE Kuanza kuwakamata na kuwatoza kiasi cha zaidi ya shilingi laki tatu bila kuangalia ni biashara gani inafanyika ni kuto watndea haki hali iliyopelekea kuwasilisha malalamiko yao kwa diwani wao.

Kufuatia hali hiyo afisa misitu wa halmashauri ya mji wa Njombe Bwana GEOFREY MWAMAKUNGE amelazimika kutoa elimu na kuwaelimisha juu ya kodi hizo ambazo wanatakiwa kuzilipa kila Julai mosi huku akisema kodi hizo zinatozwa kulingana na uwezo wa biashara.

Bwana Mwamakunge ameeleza kuwa kilichopelekea kuanza kwa msako huo ni kutokana na kufika kwa wakaguzi toka makao makuu ambao wameanza operation ya nchi nzima kuwakamata na kuwatoza wale wote ambao hawajalipia kodi za biashara zao kama Mafundi selemala,wauza mkaa,Mbao na waganga wa tiba asili.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Njombe Mjini bwana Lupyana Fute ambaye amelazimika kuwaita wataalamu hao mara baada ya kufikishiwa malalamiko toka kwa wananchi wake amesema kuwa serikali inatakiwa kuweka elimu mbele kabla ya kuanzisha msako ili kuwapa mwanga wa kutambua umuhimu wa kulipa kodi hizo.

 Aidha bwana Fute amewataka wafanyabiashara hao wanaotumia bidhaa zitokanazo na miti mjini Njombe kuanzisha umoja wao ili kupunguza gharama ya makusanyo kodi pindi msako unapoanza na kumkumba mtu mmoja mmoja.

Tuesday, November 27, 2012

VIONGOZI WILAYA YA LUDEWA WATAKIWA KUSIMAMIA MAPATO

Viongozi na Watendaji Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Hususani Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya Wakiwemo Wakuu wa Idara Mbalimbali Wametakiwa Kusimamia Mapato Kikamilifu ILi Kuiongozea Halmashauri ya Wilaya Hiyo Mapato ya Kutosha

Maagizo Hayo Yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi Baada ya Kupokea Taarifa ya Wilaya ya Ludewa Alipowasili Wilayani Hapa Kwa Ziara ya Siku Tatu Ambayo Imelenga Maeneo ya Kata Zote za Tarafa ya Mwambao

 Mkuu Huyo Wa Mkoa Alifikia Hatua Hiyo Baada ya Kubaini Wilaya Hiyo Kudumaa na Kukosa Mabadiliko Katika Nyanja Mbalimbali Ikiwemo Kilimo, Uvuvi na Biashara

Kwa Mujibu wa Ratiba, Leo Mkuu wa Mkoa Ataweka Jiwe la Msingi Katika Ofisi ya Kata ya Makonde na Kufanya Mikutano ya Hadhara Katika Kijiji cha Makonde na Lisuma. Kesho Novemba 28 Mkuu wa Mkoa Ataweka Jiwe la Msingi Katika Ujenzi wa Nyumba ya Mganga Kata ya Kilondo na Kufanya Mkuktano wa Hadhara na Kisha Kuweka Jiwe la Msingi Ofisi ya Kata ya Lundila na Kufuatiwa na Mkutano wa Hadhara

 Hata Hivyo Mkuu Huyo wa Mkoa Amewaagiza Wakuu wa Idara Hao Kusimamia na Kufuatilia na Kuacha Kukaa Maofini Badala Yake Waende Vijijini Kuwahimiza Wananchi Katika Shughuli za Maendeleo Mkuu wa Mkoa Anategemea Kumaliza Ziara Yake Novemba 29 Mwaka Huu Ambapo Atapitia Mkoani Mbeya, Kyela, Matema na Kisha Kurudi Mkoani Njombe.

Tuesday, November 13, 2012

MATOKEO YA WAJUMBE WA NEC YAVUJA DODOMA

MATOKEO ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC Uliofanyika juzi mjini Dodoma katika mkutano wa nane wa (CCM) yamevuja.

 Mwenyekiti wa chama hicho , Rais Jakaya Kikwete alitangaza jana kuwa matokeo hayo yatatangazwa leo pamoja na matokeo ya nafasi za Makamu Mwenyekiti lakini cha ajabu jana mchana zaidi ya asiliamia 90 ya wajumbe walisha jua matokeo hayo na kwa upande wa wagombea wa bara yakiwekwa na idadi ya kura zao huku Steven Wasira Akiongoza kwa kura nyingi.

 Kwa Upande wa Zanzibar Wanaodaiwa Kushinda Uchaguzi Huo ni Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto.

 Wanaodaiwa kushinda Bara Majina na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (1,967), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824)

 Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana  na Michezo, Fenela Mukangara (984).