Msako wa kodi zitokanazo na misitu uliofanyika kuanzia novemba 26 mwaka huu mjini Njombe umepelekea malalamiko makubwa kwa wafanyabiashara kuilalamikia serikali kwa kuendesha zoezi hilo kwa kutumia nguvu.
Hali hiyo imepelekea wafanyabiashara wa bidhaa zitokanazo na misitu ya maliasili kuingiwa na hofu kubwa kutokana na msako huo uliofanyika kwa kutumia jeshi la polisi ambao wamekuwa wakitumia silaha za moto huku wakisema zoezi hilo limefanika ghafla bila mawasiliano.
Wakizungumza kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Turbo baina ya Wafanyabiashara hao na maliasili wamesema kuwa hatua ya kuwakamata kulipia kodi bila kuangalia uwezo wa biashara ni kuwanyanyasa na kuwanyima haki za kufahamu sheria ya tozo la kodi hizo.
Wamesema kuwa kitendo cha Halmashauri ya mji wa NJOMBE Kuanza kuwakamata na kuwatoza kiasi cha zaidi ya shilingi laki tatu bila kuangalia ni biashara gani inafanyika ni kuto watndea haki hali iliyopelekea kuwasilisha malalamiko yao kwa diwani wao.
Kufuatia hali hiyo afisa misitu wa halmashauri ya mji wa Njombe Bwana GEOFREY MWAMAKUNGE amelazimika kutoa elimu na kuwaelimisha juu ya kodi hizo ambazo wanatakiwa kuzilipa kila Julai mosi huku akisema kodi hizo zinatozwa kulingana na uwezo wa biashara.
Bwana Mwamakunge ameeleza kuwa kilichopelekea kuanza kwa msako huo ni kutokana na kufika kwa wakaguzi toka makao makuu ambao wameanza operation ya nchi nzima kuwakamata na kuwatoza wale wote ambao hawajalipia kodi za biashara zao kama Mafundi selemala,wauza mkaa,Mbao na waganga wa tiba asili.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Njombe Mjini bwana Lupyana Fute ambaye amelazimika kuwaita wataalamu hao mara baada ya kufikishiwa malalamiko toka kwa wananchi wake amesema kuwa serikali inatakiwa kuweka elimu mbele kabla ya kuanzisha msako ili kuwapa mwanga wa kutambua umuhimu wa kulipa kodi hizo.
Aidha bwana Fute amewataka wafanyabiashara hao wanaotumia bidhaa zitokanazo na miti mjini Njombe kuanzisha umoja wao ili kupunguza gharama ya makusanyo kodi pindi msako unapoanza na kumkumba mtu mmoja mmoja.
Wednesday, November 28, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment