Tuesday, November 13, 2012

MATOKEO YA WAJUMBE WA NEC YAVUJA DODOMA

MATOKEO ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC Uliofanyika juzi mjini Dodoma katika mkutano wa nane wa (CCM) yamevuja.

 Mwenyekiti wa chama hicho , Rais Jakaya Kikwete alitangaza jana kuwa matokeo hayo yatatangazwa leo pamoja na matokeo ya nafasi za Makamu Mwenyekiti lakini cha ajabu jana mchana zaidi ya asiliamia 90 ya wajumbe walisha jua matokeo hayo na kwa upande wa wagombea wa bara yakiwekwa na idadi ya kura zao huku Steven Wasira Akiongoza kwa kura nyingi.

 Kwa Upande wa Zanzibar Wanaodaiwa Kushinda Uchaguzi Huo ni Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto.

 Wanaodaiwa kushinda Bara Majina na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (1,967), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824)

 Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana  na Michezo, Fenela Mukangara (984).

0 Comments:

Post a Comment