Serikali inatarajia kuzindua chanjo mpya mbili za watoto wachanga ikiwemo chanjo ya kuzuia kuharisha na chanjo ya kichomi NIMONIA ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayeitwa STREPTOCOCCUS PNEUMONIAE Ulioonekana kuwakumba watoto wadogo.
Akifungua kikao cha semina ya afya ya Mkoa wa Njombe iliyolenga kutoa elimu juu ya chanjo hizo mkuu wa mkoa
wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi amewataka wazazi kumpeleka mtoto kupata chanjo hizo kabla ya siku saba baada ya kuzaliwa kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kwa mtoto kutokana na kukosa chanjo hizo.
Captain Msangi ameeleza kuwa wataalamu wa afya hawana budi kutoa elimu ya kiwango cha juu kwa wauuguzi watakao husika na zoezi hilo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwani chanjo hususani za sindano zinahitaji umakini mkubwa wakati wa kumchoma mtoto.
Akitoa elimu hiyo kwa wadau mbalimbali wa afya katika ngazi ya mkoa wa Njombe Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Thomas Lujuo amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Ugonjwa wa Kuhara Umekuwa Ukishika Nafasi ya Pili Kati ya Magonjwa Yanayoongoza Kwa Kusababisha Vifo Vya Watoto Kwa Asilimia 17 Huku Ugonjwa wa Nimonia Ukisababisha Vifo Kwa Asilimia 14 Ulimwenguni Kote.
Dokta Lujuo ameeleza baadhi ya dalili za ugonjwa wa NIMONIA Kuwa ni pamoja na mtoto kupumua kwa shida,kukohoa,homa na kushindwa kula au kunyonya.
Aidha Dokta huyo amesema NIMONIA husababisha vifo zaidi ya milioni 1.4 duniani kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano huku kwa nchi za afrika,NIMONIA huchangia asilimia 18% ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Amesema Kuwa Chanjo Hiyo Ni Kampeni ya Kitaifa Inayotokana na Tafiti za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Kuonesha kuwa Watoto wengi wanapata Magonjwa ya Kuhara Na Nimonia .
Friday, November 30, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment