Saturday, January 26, 2013

Thursday, January 24, 2013

Tuesday, January 22, 2013

CHECK MY NEW RIDE: WEMA SEPETU NA GARI MPYA, ITAZAME HAPA




Picha za Gari mpya ya Wema Sepetu aina ya Audi Q7 yenye rangi nyeusi zimeonekana kwenye akaunti ya Wema ya Instagram alipokuwa beach hivi karibuni na kuiandikia caption, ‘my baby at da beach.’

Pia akaunti ya Martin Kadinda  kuna picha ya gari hiyo aliyoiandikia maneno, ‘#maisha sio manhattan…..You can creat your own Manhattan in Tz… Hata kama ni Ya muda mfupi… #Kiphating.’

Monday, January 21, 2013

MVUA YALETA KIZAAZAA MTWARA MSAADA WAHITAJIKA



 Hali ni mbaya bwawa linaendelea kujaa maji
hadi mchana huu Mali na mifugo haikusalimika na bado waathirika
walikuwa wanahangaika kujinusuru

Ni balaa kubwa la mafuriko ya maji hapa Mtwara hii leo maeneo ya
Majengo kule eneo la Chuno. Eneo hili ni karibu na nyumba ya Mzee
Hokororo au Dr Mwakipa. 

.

Hakuna taarifa yeyote ya aliyepoteza
maisha. Msaada wa haraka unahitajika kwa wananchi hawa.wa maeneo hay

Maafa stendi ya ubungo Zaidi ya magari 20 yavunjwa.



ubungo1 6ac3f
ubungo2 cc0a5
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.

Friday, January 18, 2013

Wednesday, January 16, 2013

Saturday, January 12, 2013

OLIVIA AFUNGUKA JUU YA MAISHA YAKE




Nyota wa zamani wa kundi la G-Unit, Olivia ameeleza kupanda na kushuka kwa maisha yake katika kipindi kipya cha televisheni cha Love & Hip Hop

Destiny's Child Larudi Kufanya Kazi Pamoja Tena...

      
Destininy's Child likuwa linaunundwa na Beyonce, Kelly Rowland pamoja na Michelle Williams. Kundi hilo ambalo lilifanya vizuri sana kwa miaka ya nyuma ya 1997 na ku-make headline karibu dunia nzima na baadhi ya ngoma zake mfano kama Bills, Say My Name, Survivor na nyingine nyingi ila baadae mwaka 2004 kundi hilo lilivunjika.
        Sasa latest news kutoka kwa kundi hilo ni kuwa limerudi tena na sasa hivi lipo mbioni kutoa Album yake mpya kabisa itakayokwenda kwa jina la Love Songs ambayo inatarajiwa kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu Tarehe 29.

[Picha] Hili Ndilo Jumba Analoishi Peter Wa P-Square...



       Hili ndiyo jumba la kifahari analoishi Msanii Peter wa kundi la P-Square ambapo jumba hilo lipo katika mji wa San Francisco, Marekani. Pamoja ya kuwa jumba la kifahari kama hilo pia yeye na kaka yake Paul wana jumba jingine ambalo walilijenga nchini Nigeria na kulipa jina la Squareville.
Check Nyumba Hii Ya Peter:












Thursday, January 10, 2013

Monday, January 7, 2013

MMH! ETI JUSTIN BIEBER ANAVUTA BANGI!



Kutokana na kusambazwa kwa picha kwenye mitandao zikimuonyesha Justin Bieber akivuta kitu kinachoaminika kuwa ni bangi akiwa na kikundi cha vijana wenzie

"Kila siku mtu anakuwa wa kujifunza, na najaribu kuwa kijana mwema kwa kuanguka na kuinuka tena, nimewasikia nyota wengi kamwe siataki kuwaangusha hata mmoja wao nawapenda" aliandika Bieber muda mfupibaada ya picha hizo kusambaa na watu walimiminika kutoa maoni yao kwa kumshambulia muimbaji huyo mtoto

Friday, January 4, 2013

DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU FUJO ZILIZOTOKEA WAKATI WA SHOW YAKE PAMOJA NA HASARA ILIYOPATIKANA


Usiku wa january 1 2013 Maisha Club ulikua usiku maalum kwa show ya WASAFI ambao wanaongozwa na Diamond Platnums, usiku huu umeingia kwenye Headlines baada ya fujo kubwa kutokea za kurushwa chupa, viti na mayai viza.
Noma ilianza dakika 15 baada ya Diamond kuanza kuingia kwenye stage ambapo anakiri kwamba alijua kulikua kuna watu wamepanga kuja kumfanyia fujo na aliuambia uongozi wa Maisha Club mapema kwa tahadhari na wakamwambia aendelee manake wameshaongea na wahusika lakini kumbe maongezi hayakubadilisha chochote.
Anavyosema Diamond ni kwamba waliofanya fujo ni washkaji zake wa siku nyingi ambao alikua nae Kariakoo, hao washkaji walikua wamegombana hivyo kugawanyika katika makundi mawili ambapo kundi moja lilikua linataka Diamond awe nalo alafu jingine alitenge, anasema yeye alikataa hilo wazo kwa sababu wote ni washkaji zake.
Huo msimamo ulifanya hilo kundi lililomshawishi kukasirika na kuamua kulipiza kisasi kwa kufanya fujo Maisha Club, taarifa alizipata mapema kwamba wangekuja kumzomea ambapo kweli hao jamaa walipofika Maisha wakati wa show walianza kuzomea lakini Diamond akatangaza kwa mashabiki ambao walimsupport Diamond na kupiga kelele zilizowashinda hao wazomeaji ambao baada ya kuona hivyo walianza kufanya fujo.
 
Mmoja wa hao wazomeaji ambae aliongea na millardayo usiku huo huo kwenye eneo la tukio alisema wao hawahusiki na fujo zilizotokea, waliofanya fujo ni mashabiki tu ambao pengine walichoshwa na show ya Diamond, wao walichokuja kufanya ilikua ni kuzomea tu kwa sababu Diamond alikiuka makubaliano yao.
Makubaliano yenyewe ni kwamba kwa sababu Diamond ni mshkaji wao toka kitambo kabla hajajulikana kisanii, walishakubaliana toka wakati huo kwamba akifanikiwa kimuziki inabidi asaidie na washkaji wengine wa kundi hilo ambao ni wasanii wachanga kitu ambacho jamaa wanadai Diamond hajakifanya kabisa, siku ya tukio alitakiwa kuperform na msanii mmoja wapo aitwae Papaa Masai lakini Diamond alikataa na hicho ndicho kilichowapa hasira.
Baada ya mambo kuharibika hili kundi pia limedai kwamba kuna wakati Diamond alikua anawatuma kwenda kumzomea Bob Juniour kwenye show zake na pia alikua anawatumia kwenye show zake kwenda kumshangilia.
 Diamond amesema wote waliomfanyia fujo anawajua mpaka kwa majina na tayari ameshawashitaki polisi na atahakikisha wakienda kukamatwa wanakamatwa kukiwa kuna kamera inawarekodi ili waonekane.
Kitu kingine alichokisema ni kwamba kati ya hao waliokwenda kumfanyia fujo ni pamoja na mdogo wa msanii ambae aliwahi kuwa na ugomvi nae wakapatana (huyo msanii) lakini bado huyo msanii amekua na chuki dhidi yake.
Yani Diamond aliwahi kuwa na beef na huyo msanii wakayamaliza lakini bado jamaa ana chuki, hawezi kumtaja kwa sasa na anachofanya ni kuacha uchunguzi wa polisi ufanyike kwanza, ikigundulika ni kweli atamtaja hadharani.
Kuhusu huyo msanii namkariri zaidi Diamond akisema “Uhusiano wangu na huyu msanii hauko vizuri, tulishahitilafiana kama mwaka umepita tukapatana lakini bado ana chuki dhidi yangu, tatizo niliona liliisha lakini nikaona mwenzangu kama bado ananionyesha chuki hata nikikutana nae najifanya kama hakuna tatizo lakini moyoni najua mwenzangu kuna vitu ana viendeleza vya chinichini ambavyo sivielewi”
Diamond amesema hasara ya vitu vyake kwenye hizo fujo ina thamani ya milioni zaidi ya 13 kutokana na kuibiwa simu yake ya iPhone5, cheni pamoja na camera ya video ya thamani kubwa ambayo aliinunua kwa ajili ya website yake.
CREDIT:MillardAyo

Wednesday, January 2, 2013

Eti Sajuki Alitabiri Kifo Chake! Soma Post ya Roma Hapa Kuhusu Kauli Hiyo

NINACHOKUMBUKA SHOW YA MWISHO ARUSHA YA KUMCHANGIA SAJUKI!!
TUKIWA CHUMBANI KWAKE MIMI, WASTARA, DJ CHOKA, YUSUPH MLELA NA WENGINEO, SAJUKI ALIMSHIKA MLELA MKONO HUKU AKIMTAZAMA KWA HUDHUNI NA AKAMWABIA
"SITAMALIZA SIKU 7 NITAKUWA NIMEIAGA DUNIA"
ILIKUWA HARD TYM SANA KWETU NA WENGI TULILENGWA NA MACHOZI KWA KAULI ILE!!
LEO LIMETIMIA LILE NENO...oooh god mfutie dhambi zake na muepushe na adhabu za huko!! nasisi tupate somo kuwa maisha yanaweza yakabadilika within a second!!
raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie na apumzike kwa amani!!! poleni sana marafiki wenzangu
 Pumzika kwa Amani

Alale Mahali Pema Peponi Juma Kilowoko (SAJUKI)


Ni alfjiri ya kuamkia leo katika hospitali ya Muhumbili Jijini Dar es Saalam alikokuwa amelazwa msanii wa filamu Tanzania Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki ndipo Umauti ulipomkuta.

Ni pigo lingine kwa Watanzania na wapenzi wa Filamu kwa kumpoteza msanii huyu mahiri aliyepoteza uhai baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.

Tuesday, January 1, 2013