Wednesday, January 2, 2013

Alale Mahali Pema Peponi Juma Kilowoko (SAJUKI)


Ni alfjiri ya kuamkia leo katika hospitali ya Muhumbili Jijini Dar es Saalam alikokuwa amelazwa msanii wa filamu Tanzania Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki ndipo Umauti ulipomkuta.

Ni pigo lingine kwa Watanzania na wapenzi wa Filamu kwa kumpoteza msanii huyu mahiri aliyepoteza uhai baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.

0 Comments:

Post a Comment