Sunday, December 30, 2012

Saturday, December 29, 2012

Friday, December 28, 2012

Ukweli Kuhusu Lamborghini ya Video ya Naija Girl ya Prezzo

Baada Ya Stori na picha Kusambaa ikimuonesha Prezzo akiwa na Gari la kifahari aina ya Lamborghini Team nzima ya RICHARD KADURI.blogspot.com Tuliona si mbaya Tukatafuta ukweli kuhusu Prezzo na his new Ride..
Gari hilo si la PREZZZO bali mliki halisi ni Msanii toka pande za Nigeria anayetamba na wimbo wa Skibobo alioshirikishwa mkali wa Bongo AY'(Goldie)

Bwana mkubwa ameazima mkoko huo kwa ajili ya Kushoot video ya wimbo wake wa Naija Girl...

Watu walianza kuhesabu thamani ya mali ya Prezzo kumbe Goldie ni zaidi yake..

Thursday, December 27, 2012

Wednesday, December 26, 2012

Monday, December 24, 2012

Sunday, December 23, 2012

Saturday, December 22, 2012

Friday, December 21, 2012

Wednesday, December 19, 2012

Sunday, December 16, 2012

Monday, December 10, 2012

Ray C Amshukuru Rais Kikwete kwa Msaada wa Matibabu

Msanii wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila 'Ray C'  Akiwa ameambatana  na Mama yake Mzazi Magreth Mtweve na Dada yake Sara Mtweve wamemshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa Matibabu na Kumueleza  Kuwa afya ya Mwanae imeimarika na Muda c mrefu ataendelea kupanda jukwaani.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu aliompatia ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Cortez Bryant Meneja wa Nicki Minaj Aziponda Nomination za Tuzo za Grammy

Cortez Bryant meneja wa Nicki Minaj ameziponda nomination za Tuzo za Grammy zilizotajwa siku kadhaa zilizopita ikiwa ni siku chache baada ya Meneja wa Justine Bieber Scooter Braun Kuziponda tuzo hizo kwa madai yanayofanana na ya Bryant

 Nicki Minaj pamoja na kutoa Album yake mpya hivi karibuni “Pink Friday: Roman Reloaded.” na Bieber nae kutoka na Albaum na tour yake iliyobamba zaidi 'Believe' na kuonekana kuvutia wengi lakini hawakutajwa kuwania hata category moja mwaka 2013 katika  nomination hizo.




 Cortez Bryant ambaye pia ni meneja wa Young Money Lil Wayne, Drake na Nicki Minaj aliposti katika mtandao wa kijamii wa twitter kwa kuziita "Bulls***" na alianza kwa hongera lakini akaponda utaratibu wa tuzo hizo  “Congrats to @LilTunechi and@Drake and@Hit Boy on their Grammy Noms butt....,
 Drake na Lilly Weezy wamekuwa nominated katika collabo yao ya HYFR na The Motto pia Drake binafsi amekuwa nominated kwenye category ya Best Rap Album.

Meneja  wa Biebs alitweet, "The hardest thing to do is transition, keep the train moving. the kid delivered. Huge succesful album, sold out tour, and won people over."










Nicki Minaj alikuwa nominated mara tatu katika tuzo hizo mwaka jana lakini lakini hakupata nafasi ya kuchukua tuzo hata moja. Kwa mwaka huu majina makubwa kama Lady Gaga na mwanamuziki kutoka Korea PSY mzee wa ‘Gangnam Style’ ambao watu wengi walitarajia kuonekana katika tuzo lakini hali imekuwa tofauti.      

Friday, December 7, 2012

Jay-Z, Kanye West, Frank Ocean, Black Keys waongoza Nomination list tuzo za Grammy 2013

Wasanii wa muziki wanowania za ‘Grammy awards 2013’ tuzo ambazo ni maarufu na zenye heshima kubwa Duniani, wametangazwa rasmi jumatano ya tarehe 5, December, Brindgestone Arena huko Nashville, Tennessee.




Katika nomination hizo  makundi ya muziki kadhaa na wanamuziki waliopata nafasi ya kutajwa kushindania tuzo katika cartegory zaidi ya moja ni; Jay- Z, Kanye West, Frank Ocean, Fun, na The Black Keys, Mumfrod &Sons.

K The Black Keys ni kundi la muziki wa Rock lililochaguliwa katika Cartegory tano wakati member wa kundi hilo Dan Aurbach akipata akitajwa kushindania category moja ‘non-classical producer of the year’.  The Black Keys wametajwa katika category ya Album of the Year and Best Rock Album “El Camino”, na Record of the Year, Best Rock Performance na Best Rock Song kwa wimbo wao “Loney Boy”.

Category sita zimetajwa kushindaniwa na Jay-Z na Kanye West na majina yao yaling'ara kwa sababu ya album yao ‘Watch the Throne’ waliofanya pamoja na baadhi ya kazi zao walizofanya individually.

Hizi ni tuzo za 55 za Grammy tangu zianze kutolewa na zinatarajiwa kufanyika February 10, 2013 saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Kutoka Staples Center, Los Angeles.

Baadhi ya nomination list ya tuzo hizi za Grammy 2013.

Album Of The Year:
•             "El Camino" - The Black Keys
•             "Some Nights" - Fun.
•             "Babel" - Mumford & Sons
•             "Channel Orange" - Frank Ocean
•             "Blunderbuss" - Jack White

Record Of The Year:
•             "Lonely Boy" - The Black Keys
•             "Stronger (What Doesn't Kill You)" - Kelly Clarkson
•             "We Are Young" - Fun. featuring Janelle Monae
•             "Somebody That I Used To Know" - Gotye featuring Kimbra
•             "Thinkin Bout You" - Frank Ocean
•             "We Are Never Ever Getting Back Together" - Taylor Swift

Best New Artist:
•             Alabama Shakes
•             Fun.
•             Hunter Hayes
•             The Lumineers
•             Frank Ocean

Song Of The Year:
•             "The A Team" - Ed Sheeran
•             "Adorn" - Miguel
•             "Call Me Maybe" - Carly Rae Jepsen
•             "Stronger (What Doesn't Kill You)" - Kelly Clarkson
•             "We Are Young" - Fun.

Best Pop Solo Performance:
•             "Set Fire to the Rain (Live)" - Adele
•             "Stronger (What Doesn't Kill You)" - Kelly Clarkson
•             "Call Me Maybe" - Carly Rae Jepsen
•             "Wide Awake" - Katy Perry
•             "Where Have You Been" - Rihanna

Best Rock Album:
•             "El Camino" - The Black Keys
•             "Mylo Xyloto" - Coldplay
•             "The 2nd Law" - Muse
•             "Wrecking Ball" - Bruce Springsteen
•             "Blunderbuss" - Jack White

Best Rock Song:
•             "Freedom at 21" - Jack White
•             "I Will Wait" - Mumford & Sons
•             "Lonely Boy" - The Black Keys
•             "Madness" - Muse
•             "We Take Care of Our Own" - Bruce Springsteen

Best R&B Album:
•             "Black Radio" - Robert Glasper Experiment
•             "Back to Love" - Anthony Hamilton
•             "Write Me Back" - R. Kelly
•             "Beautiful Surprise" - Tamia
•             "Open Invitation" - Tyrese Gibson

Best R&B Song:
•             "Adorn" - Miguel
•             "Beautiful Surprise" - Tamia
•             "Heart Attack" - Trey Songz
•             "Pray for Me" - Anthony Hamilton
•             "Refill" - Elle Varner

Best Rap Album:
•             "Take Care" - Drake
•             "Food and Liquor 2: The Great American Rap Album Pt. 1" - Lupe Fiasco
•             "Life Is Good" - Nas
•             "Undun" - The Roots
•             "God Forgives, I Don't" - Rick Ross
•             "Based on a T.R.U. Story" - 2 Chainz

Best Rap Song:
•             "Daughers" - Nas
•             "Lotus Flower Bomb" - Wale featuring Miguel
•             "Mercy" - Kanye West featuring Big Sean, Pusha T & 2 Chainz
•             "The Motto" - Drake featuring Lil Wayne
•             "N****s in Paris" - Jay-Z & Kanye West
•             "Young, Wild & Free" - Snoop Dogg & Wiz Khalifa featuring Bruno Mars

Best Country Album:
•             "Uncaged" - Zac Brown Band
•             "Hunter Hayes" - Hunter Hayes
•             "Living for a Song: A Tribute to Hank Cochran" - Jamey Johnson
•             "Four the Record" - Miranda Lambert
•             "The Time Jumpers" - The Time Jumpers

 Tembelea  Website ya Grammy kwa Nomination list nzima:

Monday, December 3, 2012

 Movie ya ‘Expendable 2’yaburuzwa tena mahakamani, ni baada ya mlipuko wa ukweli uliomuua actor mmoja na kumjeruhi vibaya actor mwingine
 Expendable two iliyowashirikisha action movie stars kibao wakiongozwa na Sylvester Stalonne (Rambo), Jean Claude Vanndamme, Jet-Li, Arnold ShwazNiger, na wengine, imekumbana na tatizo la kisheria.
Waandaaji na wawezeshaji wengine wanakabiliwa na mashtaka yanayotokana na scene ambayo haikwenda sawa na kupelekea mtu mmoja kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Nuo Sun alijeruhiwa vibaya katika mlipuko ambao ulisababisha kifo cha muigizaji Kun Liu, ambapo kwa mara ya kwanza familia ya marehemu iliiburuza mahakamani ‘Expendable 2’ wakidai fidia mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha kiasi cha dola za marekani 25,000.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Nuo Sun ambae alijeruhiwa vibaya na kupelekwa jijini Munich huko Ujerumani kwa matibabu akiwa chini ya the best specialist amewafungulia mashtaka waandaaji na washiriki wengine wa movie hiyo.

Katika mashitaka hayo yenye kurasa 12 Sun amedai kuwa, “mlipuko na similar extra-hazardous activities vilisababisha tukio la hatari juu ya rubber boat wakati wa kushoot sehemu ya pili ya filamu hiyo October 27, 2011.

“Kwa uzembe wa moja kwa moja wa washitakiwa, kutojali, na matendo kinyume na sheria, mlalamikaji aliumia na kupata majeraha katika afya yake, uwezo wa kufanya kazi, mshituko wa kiasi kikubwa na majeraha katika mfumo wake wa fahamu, shingo, kichwa, mwili, mikono na miguu, majeraha yote haya yanaweza kuwa ya kudumu, na majeraha haya yamesababisha na yanaendelea kusababisha madhara katika fahamu zake na mwili wake kwa ujumla. Hivyo mlalamikaji anadai fidia .” Haya ni baadhi ya maandishi yanayopatikana kwenye faili la mashtaka lenye kurasa 12.

Akiwakilishwa na Robert M. Klein, Sun anadai fidia ya hasara ya kipato chake kwa wakati uliopita, uliopo na ujao. Lakini pia anadai fidia ya jumla zaidi ya $25,000, gharama za matibabu ya wakati uliopita, uliopo na hata baadae, gharama za kuendesha kesi na mengine ambayo mahakama itaamua.

Baada ya mlipuko huo ulioua mmoja kati ya actors wa movie hiyo na kumjeruhi vibaya Sun, uongozi na watayarishaji wa movie hiyo walitoa tamko kuomba radhi na kuwaitakia pole familia ya marehemu na vilevile kuendelea kusapoti kwa karibu sana familia na kumhudumia Sun akiwa hospitalini.

Hata hivyo Sun alikanusha kauli iliyotolewa na waandaaji hao kuwa Jet-Li alikuwa pia karibu na mlipuko huo, na kusema hakuna star yoyote aliyekuwa karibu na mlipuko huo

Chanzo Leotainment

Sunday, December 2, 2012

GAGA APOSTI PICHA AKIWA NA SIMBA SOUTH AFRICA


Lady Gaga amepata shavu la kutalii vivutio vya Afrika baada ya kudondoka Afrika Kusini alikokuwa kwa ajili ya tour yake na kutembelea mbuga za wanyama

Lady Gaga alionesha furaha yake ya kukutana uso kwa uso na kupiga picha na wanyama wakali simba na kupost picha hizo kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa amevalia nguo zenye rangi yanayoendana na mzingira ya hapo nyuma yake wakionekana simba kadhaa wakiwa wamejiachia kwenye nyasi kama






Gaga aliposti picha zake zikiwa na yanayosema SAFARI PICTURE: na yanayoeleza umbali wa futi 10 kutoka pale walipo simba13 na watoto 2.

‘The bad Romance singer’alipost picha kupitia twitter inayoonyesha akiwa kavaa mavazi ambayo yanaendana kabisa na nature ya pale alipo na  vile hakuna binadamu maeneo yale. "Nilispend nao takribani dakika 30 na kupiga picha!”

“hii niliichukuwa kama futi 5 hivi kutoka kwa simba jike, isn’t she beautiful!”

“simba walijiskia poa hata wakaamka at one point na wakatufanya kuwasogelea zaidi.”

Saturday, December 1, 2012

WANANDOA HATARINI KUAMBUKIZWA VVU

Watu Waanoishi Katika Ndoa Wapo Katika Hatari Kubwa ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kwa Asilimia 70 Kwa Kuwa Ndio Wanaoongoza Kutoka Nje ya Ndoa Hivyo Kusababisha Ongozeko la WatotoYatima

Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi  Katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Yaliyofanyika Katika kata ya Mji Mwema Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

Akizitaja Sababu  za Ongezeko la maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Mkuu Huyo Amesema Kuwa Ngono Zembe Ulevi, Kurithi Wajane na Wagane na Wanaume Kutotahiriwa. Pia Amezitaja Sababu Zingine Kuwa Ni Matumizi mabaya ya Nyumba za Kulala Wageni Ufahamu Mdogo Juu ya Matumizi ya Kinga na Matumizi Hafifu ya Kinga.

Pia Mkuu wa Mkoa Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kuwanyang'anya Leseni Wamiliki wa Nyumba za Kulala Wageni Watakaokiuka Maadili ya Leseni Hizo

Kulingana na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi Wana Haki Sawa na Wale Ambao Hawajaambukizwa Hivyo Kumnyanyapaa Mwenye Virusi vya Ukimwi ni Kosa Kisheria.

Amesema Lengo la Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Dunia ni Kupata Fursa ya Kutafakari Kwa Undani Ukubwa wa Tatizo la VVU na Ukimwi na Madhara ya Janga Hili kwa Jamii Zetu na Kujua mikakati, Mafanikio na Changamoto za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.

Akisoma Risala Mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Amesema Kuwa Takwimu Zinaonesha Kuwa Jumla ya Watu 2161 Kati ya Watu 21053 Sawa na Asilimia 10 ya Watu Walijitokeza kupima kwa Hiari katika Kipindi cha Kuanzia Julai 2011 hadi Juni 2012  Walikutwa na Maambukizi