Wasanii wa filamu nchini wamelalamikia kudharaulika pale wanapopewa ujira mdogo kuliko wale wangine mbao pengine hucheza sehemu ndogo na kudai wadau wa tasnia hiyo waelimishwe juu ya kazi hiyo
Kauli hiyo iliyotolewa na msanii wa fani hiyo ya uchekeshaji Hamisi Changare 'Mtanga' inaonyesha ina ukweli ndani yake kwa kupewa ujira mdogo kwenye filamu zingine huku wakishindwa kuthaminiwa na kuheshimiwa
Mtanga anasema kuwa anadhani kuwa kudharaulika kwao anahisi kunatokana na uchekeshaji wao au uchezaji wao wa sehemu ndogo katika filamu ambazo uhusika wake hauna maana sana kama wafunguaji geti au wafanya kazi wa ndani hivyo inachangia kwa kiasi kikubwa kutopewa heshima
"Fani yetu imekuwa ngumu sana sijui kwa nini wadau wamekuwa wakidharau sana, tatizo kubwa lipoi kwenye malipo wengi huwa wanashindwa kufanya kazi ya mtu kwa sababu wanacholipwa tofauti na kazi anayofanya hivyo bado tuna nyonywa tena kwa kiasi kikubwa" Alisema Mtanga.
Wednesday, December 26, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment