Padri Apigwa Risasi na Watu Wasiojulikana Zanzibar
Father Ambros Mkenda wa Parokia ya Mpendae katika Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
0 Comments:
Post a Comment