Saturday, December 1, 2012

WANANDOA HATARINI KUAMBUKIZWA VVU

Watu Waanoishi Katika Ndoa Wapo Katika Hatari Kubwa ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kwa Asilimia 70 Kwa Kuwa Ndio Wanaoongoza Kutoka Nje ya Ndoa Hivyo Kusababisha Ongozeko la WatotoYatima

Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi  Katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Yaliyofanyika Katika kata ya Mji Mwema Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

Akizitaja Sababu  za Ongezeko la maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Mkuu Huyo Amesema Kuwa Ngono Zembe Ulevi, Kurithi Wajane na Wagane na Wanaume Kutotahiriwa. Pia Amezitaja Sababu Zingine Kuwa Ni Matumizi mabaya ya Nyumba za Kulala Wageni Ufahamu Mdogo Juu ya Matumizi ya Kinga na Matumizi Hafifu ya Kinga.

Pia Mkuu wa Mkoa Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kuwanyang'anya Leseni Wamiliki wa Nyumba za Kulala Wageni Watakaokiuka Maadili ya Leseni Hizo

Kulingana na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi Wana Haki Sawa na Wale Ambao Hawajaambukizwa Hivyo Kumnyanyapaa Mwenye Virusi vya Ukimwi ni Kosa Kisheria.

Amesema Lengo la Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Dunia ni Kupata Fursa ya Kutafakari Kwa Undani Ukubwa wa Tatizo la VVU na Ukimwi na Madhara ya Janga Hili kwa Jamii Zetu na Kujua mikakati, Mafanikio na Changamoto za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.

Akisoma Risala Mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Amesema Kuwa Takwimu Zinaonesha Kuwa Jumla ya Watu 2161 Kati ya Watu 21053 Sawa na Asilimia 10 ya Watu Walijitokeza kupima kwa Hiari katika Kipindi cha Kuanzia Julai 2011 hadi Juni 2012  Walikutwa na Maambukizi  
   

0 Comments:

Post a Comment