Monday, May 8, 2017

ALICHOONGEA JOSE MOURINHO BAADA YA KUFUNGWA NA ARSENAL


Jose Mourinho anaamini wachezaji wake walicheza vizuri licha ya kutopata ushindi, amedai pamoja na ushindi wao Arsenal hawakuwa bora zaidi ya United

Jose Mourinho amesema hawezi kuwalaumu wachezaji wake wa Manchester United kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Arsenal, akidai kuwa 'hakuweza kuwataka wacheze zaidi'.

Mreno huyo alibadili kikosi chake kwa kiwango kikubwa katika ziara yao ya Emirates, akifanya mabadiliko nane katika kikosi kilichoikabili Celta Vigo na kushinda 1-0 juma lililopita.

Bila ya wachezaji wengi muhimu, United iliangukia pua kwa kipigo cha 2-0 mjini London kupitia mabao kutoka kwa Granit Xhaka na Danny Welbeck, lakini Mourinho hakuona sababu ya kulaumu yeyote katika timu yake.

"Napenda viwango vya wachezaji binafsi na timu kwa ujumla pia," alikiambia Sky Sport News. "Tumefungwa kwa sababu hatukufunga na tulipata nafasi nzuri kufunga kabla yao.

"Walikuwa na bahati kufunga. Siwezi kuwadai zaidi wachezaji wangu ambao hawakucheza hata dakika moja wiki kadhaa - Phil Jones Chris Smalling na Juan Mata walicheza vizuri.

"Timu yangu ilikuwa nzuri, imejipanga vema, tulijaribu kushinda, tulicheza kutafuta ushindi, tulikaba vema, na Arsenal hawakuwa bora kuliko sisi kwa mtazamo wangu."

United ambao walishuhudia mwendo wao wa mechi 25 bila kufungwa ukifika mwisho mikononi mwa Arsenal, watarejea dimbani Alhamisi kwa mechi ya marudiano hatua ya nusu fainali Ligi ya Uropa dhidi ya Celta Vigo.

0 Comments:

Post a Comment