Sunday, May 7, 2017

SIMBA YARUDI KILELENI LIGI KUU



Simba imerudi kileleni baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon

Simba imeezidi kuitia presha Yanga katika kutetea ubingwa wake wa ligi ya Vodacom baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon.

Ushindi wa leo umeirudisha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 62 na kuoacha Yanga kwenye nafasi ya pili wakiwa na poonti 59 lakini wakiwa na michezo miwili mkononi.
Mshambuliaji Ibrahim Ajibu alianza kuifunhia Simba bao la kuongoza dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza kufuatia shuti kali la mabali ambalo lilimgonga beki wa African Lyon na mpira kupoteza mwelekeo na kutinga wavuni.

0 Comments:

Post a Comment