Wednesday, May 3, 2017

Simba kudai point 3 FIFA, yatoa rai kwa FA Cup

Rais wa club ya simba Evans Aveva ameonesha wasiwasi wake wa kutopata haki ya point 3
na magoli 3 kutoka kwa Kagera Sugar baada ya kamati ya katiba na sheria na hadhi ya wachezaji kuzirejesha point hizo kwa Kagera Sugar kwa madai ya kuwa Simba haikufuata utaratibu.

Aveva amesema kuwa kanuni iliyopo ilipaswa kufuatwa hata pasipo wao kukata rufaa.

Kutokana na sakata hilo Simba sasa wanasubiri barua ya kupokwa point hizo kutoka bodi ya ligi na kuahidi kulifikisha suala hilo FIFA baada ya kufanya tathimini.

Simba wataambatanisha pia kesi ya usajili ya mchezaji Baraka Yusuphu aliyesajiliwa na Simba na kumtoa kwa mkopo kwa Kagera Sugar, hivyo alistahili arudi kuichezea simba kwa msimu huu.

Kesi ambayo hawajui hatma yake ni nini kutoka kamati ya sheria na katiba na hadhi ya wachezaji ingawa kadi ya usajili ya Mbaraka Yusuphu iliyoidhinishwa na TFF inaonesha ni mchezaji wa Simba

Pia Simba imetoa rai kwa waendeshaji na wadhamini wa mashindano ya FA yapewe heshima kwa kutoa taarifa za viwanja mapema na sio kusubiri dakika za mwisho kufuatia kubadilisha maamuzi ya uwanja upi utatumika kwa ajili ya fainali za mashindano hayo dhidi ya timu na Mbao Fc ya jijini Mwanza.

Amezungumzia pia sakata la kufungiwa kwa msemaji wa club hiyo Haji Manara na kusema kuwa uamuzi umetolewa haraka sana wakati TFF haijasikiliza maelezo ya Manara hivyo Haji Manara amepeleka maombi ya kupitia upya kesi hiyo

0 Comments:

Post a Comment