
AmissiTambwe na Obrey Chirwa jana wameirudisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi ya Vodacom
baada ya kufunga mabao mawili nambayo yameifanya timu hiyo kufikisha pointi 59 sawa na Simba.Ushindi wa jana unaweza kuwa wa muda kwa Yanga kukaa kileleni mwa msimamo kwani Simba leo watashuka uwanja wa taifa kucheza na African Lyon.
Yanga ambayo imetoka kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho hadi mapumziko ilikuwa bado haijapata bao na kuzua hofu kwa mashabiki wake ambao walikuwa wanasubiria bao muda wowote. Hadi dakika 90 za mchezo yanga waliweza kuibuka na ushindi wa bao mbili kwa bila.
0 Comments:
Post a Comment