Katika mkutano na waandishi, Wenger alibainisha kuwa Lucas Perez hatacheza kwenye kikosi chake kadhalika Xhaka hatacheza dhidi ya Man United
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa kiungo wake Granit Xhaka hatacheza dhidi ya Manchester United wikiendi ijayo.
Licha ya maoni mbalimbali tangu alipotua Emirates akitokea Borussia Monchengladbach msimu uliopita majira ya joto, Xhaka ameanza mechi 33 katika michauno yote msimu huu lakini ataukosa mchezo utakaopigwa kunako dimba la Emirates Jumapili.
Katika mechi waliyofungwa 2-0 na Tottenham Hotspur, Mswisi huyo alikwatuliwa kwenye kifundo cha mguu na ingawa aliendelea hadi dakika ya 65, ameshindwa kufanya mazoezi wiki hii.
Kulingana na maelezo yake kwenye mkutano na waandishi wa habari, Wenger alibainisha kuwa Lucas Perez hatacheza kwenye kikosi chake licha ya kufanya mazoezi siku kadhaa zilizopita, lakini kulikuwa na habari njema kuhusu Shkodran Mustafi.
Beki huyo wa kati amekosekana tangu Aprili 10, lakini Wenger amedokeza kuwa anaweza kucheza sasa baada ya kufanya mazoezi ya kawaida.
0 Comments:
Post a Comment