Wednesday, May 10, 2017

JAJI MAHAKAMA KUU ATUPWA JELA INDIA

Jaji wa mahakama kuu ya Calcutta nchini India Chinnaswamy Swaminathan amehukumiwa kifungo cha
miezi sita jela. 
Katika historia ya nchi hiyo, Swaminathan anakuwa jaji wa kwanza wa mahakama ya juu kuhukumiwa kwenda jela. 
Jaji Swaminathan alikutwa na hatia ya kudharau mahakama baada ya hatua yake ya kutaka kumhukumu jaji mkuu wa India na majaji wengine sita wa mahakama ya juu kifungo cha miaka mitano jela. 
Mnamo mwezi Januari mwaka huu, Jaji huyo aliwashutumu baadhi ya majaji wa juu kuwa ni mafisadi. 
Jaji Karnan alimwandikia waziri Mkuu waraka maalum akitaka kuungwa mkono kwa juhudi zake na kutaka majaji hao wa mahakama wakamatwe, wachunguzwe na kutupwa jela miaka tano kwa madai ya ufisadi.
Lakini Jaji Karnan hakutoa ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba hao wakubwa zake ni wafisadi. Hivyo kupelekea Jaji mkuu wa nchi hiyo katika siku za hivi karibuni ametoa agizo kwamba jaji huyo apelekwe hospitali kupimwa akili kwani alisema wanadhani kwamba si mzima wa akili.

0 Comments:

Post a Comment