Sunday, May 7, 2017

KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA VS AFRICAN LYON


Kocha wa Simba, Joseph Omog Leo Jumapili atakuwa na kazi moja ya kuhakikisha wanaifunga African Lyon
na kurudi kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi ya Vodacom.

Pambano hilo litapigwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 10 za jioni.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0, katika mchezo wa kwanza uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Simba imepania kutwaa ubingwa msimu huu hivyo itaingia kwa nguvu kwenye mchezo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya ubingwa.

Kocha Omog anafurahia kiwango bora kilichoonyeshwa na vijana wake katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Azam FC na ametamba kuifunga Lyon leo.

Katila kikosi cha kesho Omog ataendelea kumkosa beki Method Mwanjali aliyepo nje kwa mwezi wa pili sasa akiuguza goti lakini anajivunia kurejea kwa Abdi Banda ambaye awali alisimamishwa na Bodi ya Ligi kutokana na kumpiga ngumi kwa makusudi George Kavila wa Kagera Sugar.

0 Comments:

Post a Comment