Wednesday, May 31, 2017

IGP SIRO ATANGAZA DAU LA MILIONI 10 RUFIJI


Dar es Salaam. Mkuu mpya wa jeshi la polisi, IGP Simon Sirro amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari leo,  na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. 


“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.

Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi. “Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema

0 Comments:

Post a Comment