Ligi kuu nchini Englang inaendelea wiki hii ambapo itapigwa michezo kadhaa.
Ikiwa ni mechi za kumalizia msimu huu wa 2016/2017 bado kitendawili cha ubingwa ni kigumu ingawa Chelsea anapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo. Jana ulipigwa mchezo mmoja ambapo Tottenham walikipiga na West Ham United na wakapoteza mchezo huo kwa kufungwa goli moja lililofungwa kipindi cha pili dakika ya 65 na Manuel I Lanzini.Matokeo hayo yanaongeza kuipa nafasi kubwa Chelsea ya kutwaa ubingwa huo ingawa ligi bado na kwenye mchezo wa mpora wa miguu lolote linaweza kutokea.
Chelsea ambao ni vinara katika msimamo wa ligi hilo watakipiga juma tatu ya tarehe 8 dhidi ya MIDDLESBROUGH katika dimba la Stamford Bridge. Hivyo Chelsea wanahitaji ushindi wa aina yeyote ili kujiweka nafasi salama katika harakati za kutwaa ubingwa was ligi hilo.
0 Comments:
Post a Comment