Saturday, May 13, 2017

CHELSEA BINGWA LIGI KUU UINGEREZA



Chelsea sasa wameshinda mataji matano ndani ya miaka 13 iliyopita, rekodi inayofikiwa na Manchester United pekee

Meneja wa Chelsea Antonio Conte ameelekeza shukrani zake za dhati kwa wachezaji wake baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza 2016-17 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Muitaliano huyo ameelezea ushindi huo kama "mafanikio makubwa" na ameshukuru umoja baina yao na mashabiki, kampeni za kukumbukwa katika Stamford Bridge.




"Asanteni, asanteni. Haya ni mafanikio makubwa kwa wachezaji. Nawashukuru sana kwa mafanikio na kazi njema waliyofanya. Wamenionyesha moyo wa kujituma na kujitahidi kupata mafanikio makubwa msimu huu. Baada ya ushindi huu ni lazima tuwe na furaha, tumefurahi sana," Conte alikiambia Sky Sports News.

"Kila mechi nahisi kama nimecheza na wachezaji wangu! Nonyesha mapenzi na nia, na hamu ya kuendelea kubaki na wachezaji wangu katika kila wakati wa mchezo. Huyo ndiye mimi, ndivyo nilivyo.

"Kwa wakati uliopo, uliopita, nadumu na wachezaji wangu katika hali ngumu na nzuri. Tumetwaa taji hili pamoja."

Michy Batshuayi akitokea benchi alikuwa shujaa wa Chelsea kwa kufunga goli ambalo liliwazamisha West Brom na kutwaa taji dakika ya 82.



Winga wa Chelsea Eden Hazard naye hakuwa na sababu ya kuchelewa kumshukuru na kumpongeza meneja wake Antonio Conte kwa kuiongoza klabu kutwaa taji la Ligi ya Uingereza mbele ya West Bromwich Albion usiku huu.

"Inapendeza kushangilia na mashabiki. Mechi ilikuwa ngumu sana. Tuna furaha sana," alisema Hazard.

"Tumeongea mengi kuhusu meneja tayari, ni mtu mwema sana na tunafanya naye kazi sana kwenye mazoezi. Nampongeza yeye pamoja na wachezaji. Tulifungwa na Arsenal na tukaenda mwendo wa ushindi. Na hapo ndipo tuliposema tunaweza kushinda ubingwa wa ligi."

Chelsea sasa wameshinda mataji matano ndani ya miaka 13 iliyopita, rekodi inayofikiwa na Manchester United pekee.

0 Comments:

Post a Comment