Friday, May 12, 2017

MISIMU 10 BORA YA CHRISTIANO RONALDO


Cristiano Ronaldo amekuwa na misimu mizuri sana tangu akiwa Sporting ya nchini Ureno na hadi sasa akiwa Real Madrid, leo tunakuletea misimu 10 bora ya Mreno huyo toka aanze kucheza soka la kulipwa.


10.2009/10. Huu ndio msimu ambao Ronaldo alinunuliwa kwenda Madrid kwa rekodi ya dunia na msimu wake wa kwanza aliwasha moto mkubwa kwa kufunga mabao 26 katika michezo 29 ya La Liga na kufunga mabao 33 katika michezo 35 jumla aliyoichezea Madrid lakini hakupata kombe.

09.2006/07.Msimu huu akiwa Manchester United, Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao 17 katika michezo 34 aliyoichezea United ligi kuu na akafunga 3 Champions league na kufanikiwa kubeba taji la ligi kuu.

08.2008/09.Msimu bora zaidi kwake akiwa United na ndio msimu ulioacha Madrid wamnunue, Ronaldo msimu huu alipga goli 18 katika ligi kuu, akafunga 4 Champions League akashinda kombe la ligi na klabu bingwa dunia.

07.2012/13.Akiwa Real Madrid msimu huu Ronald alifanikiwa kufunga mabao 34 kati ya mechi 34 za ligi kuu, akafunga 12 kati ya 12 champions leaguena jumla alifunga mabao 55 katika mechi 55 lakini hakubeba kombe.

06.2014/15. Ronaldo bado yuko Real Madrid ambapo msimu huu walibeba klabu bingwa dunia huku akifunga mabao 48 kati ya mechi 35 za ligi kuuna mabao 10 kati ya mechi 12 za champions league.

05.2010/11. Msimu huu Ronaldo aliipa Madrid kombe la Copa Del Rey na alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 53 katika mechi 54 alizoichezea Madrid katika msimu huu.

04.2007/08. Huu ni msimu ambao nina uhakika Ronaldo hawezi kuusahau, alikuwa akiichezea Manchester United na akafunga mabao 31 katika ligi kuu huku jumla akifunga mabao 42 kati ya michezo 49 na kuipa United kombe la ligi kuu na Champions league.

03.2011/12. Ronaldo hapa yuko Real Madrid akafunga mabao 46 katika mechi 38 La Liga huku akifunga jumla ya mabao 60 katika michezo 55 na kufanikiwa kubeba kombe la La Liga.

02.2013/14. Msimu huu Ronaldo aliifanya Real Madrid ing’are kwani jumla ya mabao 51 katika michezo 47 aliyoichezea Real Madrid na hii ilitosha kuwapa Madrid kombe la Champions League na Copa Del Rey.

01.2015/2016. Hakika Ronaldo anaweza kusahau vyote ila sio msimu huu, na mwenyewe amekiri kwamba huu ndio msimu bora katika maisha yake ya soka, alifunga mabao 51 katika michezo 48  aliyoichezea Real Madrid na kuipa kombe la Champions League lakini msimu huu alipata kitu kipya na kikubwa ambacho ni kuipa Ureno ubingwa wa Ulaya.

0 Comments:

Post a Comment